
YANGA imepanga kuwaanzisha nyota wake wote leo katika mchezo wao wa Kombe la FA watakaokipiga na Iringa United kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.
Kocha wa Yanga, Charles Mkwasa amesema haifahamu Iringa lakini anaamini ni timu nzuri hivyo yeyeatakwenda kwenye mchezo huo akiwa na kikosi kizima ili aweze kupata ushindi na kwenda hatua inayofuata.
“Maandalizi yetu ni mazuri tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi ili tuweze kutinga hatua nyingine inayofuatia ya michuano hii.

“Iringa United siijui lakini ni timu nzuri na tunaiheshimu kama tunavyoziheshimu timu nyingine, tutaingia uwanjani kwa lengo moja tu la kupambana kwa nguvu zetu zote,” alisema Mkwasa na kuongeza:
“Nitawatumianyota wangu wote kwani mechi hii ni ya mtoano, tukifungwa tu ndiyo tumetupwa nje ya michuano kwa hiyo lazima nyota wangu wote wacheze.