×

Harmonize Apagawisha Tamasha la Mziki Mnene Dar

Msanii wa bongo Fleva Harmonize akitoa burudani katika Tamasha la Muziki Mnene lililofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar usiku wa kuamkia leo.
Harmonize na mpenzi wake Sara wakiwa mbele ya mashabiki.

Usiku wa kuamkia leo mashabiki wa burudani walipata burudani nya aina yake kwenye tamasha la Muziki Mnene lililofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar.

Katika tamasha hilo wanamuziki mbalimbali walipiga shoo ambapo miongoni mwao ni Kundi la Weusi, MwanaFA, Dogo Aslay, Mzee wa Bax, Man Fongo, Richa Mavoko na wengineo.

Mabaunsa wakiwa wameimarisha ulinzi wakati Harmonize akitaka kushuka jukwaani.

Shoo ilimalizwa na Abdul Kahali ‘Harmonize’ Konde Boy ambaye alipiga shoo ya kufuru huku akimpandisha jukwaani Baby wake Sara na kupeana naye mahaba laivu jukwaani.

Wasanii wanaounda kundi la Weusi, Joh makini (kushoto), Nick wa Pili (kulia) na G-Nako (katikati) wakitoa burudani katika Tamasha la Muziki Mnene lililofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar usiku wa kuamkia leo.
Sehemu ya mashabiki.
Lord Eyez (kulia) na Joh Makini wakichana.
Mashabiki wakifuatilia burudani.
Dogo Aslay akifanya yake
Man Fongo (Mwenye kofia)  na akiwa na wasanii wa Harmonize.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

Leave a Comment