
Vita ni vita! Kama uliamini vita kati ya wasanii wawili wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny na Rajabu Abdul au Harmonize imemalizika, basi unajidanganya kwani ndiyo kwanza ni mbichi.
Wasanii hao walianza kutofautiana baada ya Harmonize au Harmo kuondoka kwenye Lebo ya WCB chini ya Diamond Platnumz.
Vita yao ilikuwa kali zaidi pale ilipovuja video ya kimahaba ya Rayvanny na mrembo Paula Kajala ambapo Harmonize alimsindikiza kufungua jalada la kesi Polisi mama wa Paula, Kajala Masanja ambaye alikuwa mpenzi wake.

Hata hivyo, siku chache Rayvanny naye akadaiwa kuvujisha video chafu ya Harmonize akimtaka kimapenzi Paula na kukoleza vita yao.
Kama hiyo haitoshi, mara baada ya Harmonize kuanza kujiita Tembo, ghafla Rayvanny naye aliibuka akijiita Chui.
Huku na huku kuna kipindi Harmopnize alijiita Teacher, ghafla Rayvanny akaibuka na kujiita Lecturer akimaanisha mwalimu wa chuo.
Sasa; mambo yamekuwa mambo kwani mara baada ya Harmonize kujiita Bakherssa (tajiri mkubwa Tanzania), Rayvanny ameibuka na kujiita Bill Gates (tajiri mkubwa duniani).
Inavyoonekana, kasumba ya wasanii wa Bongo kujiita majina ya wanyama huwenda sasa ikapotea baada ya baadhi yao kuelekeza nguvu zao kujiita majina ya matajiri au wafanyabiashara maarufu duniani.
Wakati Harmonize akitaka kuitwa jina la mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu ya Azam, Said Salim Bakhresa, Rayvanny yeye anataka aitwa jina la Bill Gates tajiri na mfanyabiashara maarufu duniani.
Lakini hayo yote yanakuja baada ya Diamond kuwa anajiita Dangote; tajiri namba moja barani Afrika, Harmonize Bhakresa na Rayvanny Bill Gates hivyo mpambano unaendelea.
Ikumbuke katika upande wa majina ya wanyama, Diamond ni Simba, Harmonize ni Tembo, Rayvanny ni Chui, Young Lunya ni Mbuzi, Shetta na Dudu Baya ni Mamba, Country Wizzy ni Fisi, Wema Sepetu ni Twiga na wengineo.
Stori; Mwandishi Wetu, Dar