×

Mbappe; Mtoto Anayefanya Mambo ya Wakubwa

 

MARA chache sana unaweza kumuamini mtoto kufanya mambo makubwa. Mara nyingi watoto huaminika kufanya mambo ya kitoto, lakini Kylian Mbappe ni mtoto anayefanya mambo ya kikubwa.

 

Staa huyu wa PSG juzi Ijumaa alifikisha umri wa miaka 21 lakini hata kabla hajafikisha miaka 20 alikuwa ameshafanya mambo makubwa. Juzi kafikisha miaka 21 na miguu yake inaonekana haijalegea. Bado ana nguvu. Bado damu inachemka.

 

Tayari akiwa mtoto mdogo kabisa ameshashinda Kombe la Dunia, makombe matatu ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) na akiwa amefunga zaidi ya mabao 100, yakiwemo 19 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Tangu alipofungua akaunti yake ya mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na miaka 18, katika mchezo wa Monaco wa raundi ya 16 bora ugenini dhidi ya Manchester City Februari 21, 2017, Mbappe amefanya mambo makubwa baada ya hapo.

 

Alimaliza msimu huo akiwa na mabao sita wakati Monaco ilipofika nusu fainali msimu huo na amefunga zaidi ya mabao kumi akiwa na Paris Saint- Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

MABAO MENGI KWENYE LIGI YA MABINGWA ULAYA KABLA MCHEZAJI HAJAFIKISHA MIAKA 21

REKODI:

19 Kylian Mbappé (Monaco/Paris Saint-Germain)

12 Karim Benzema (Lyon)

9 Patrick Kluivert (Ajax)

8= Obafemi Martens (Internazionale Milano)

8= Lionel Messi (Barcelona)

8= Raúl González (Real Madrid)

8= Javier Saviola (Barcelona)

8= Erling Braut Haaland (Salzburg)*

7= Thierry Henry (Arsenal)

6= Cesc Fàbregas (Arsenal)

6= Lars Ricken (Borussia Dortmund)

*Hafikishi miaka 21 hadi Julai 2021

 

MATAJI YA MBAPPE:

Ubingwa Kombe la Dunia (2018)

Ubingwa michuano ya Ulaya ya U-19 (2016)

Monaco;

Ubingwa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) (2016/17)

Paris Saint-Germain;

Ubingwa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) (2017/18, 2018/19)

Ubingwa Kombe la Ufaransa (2017/18)

Ubingwa Kombe la Ligi Ufaransa (2017/18)

 

 

TUZO BINAFSI:

2016 – Aliingia kwenye kikosi bora cha Euro U-19

2016/17 – Aliingia kwenye kikosi bora cha msimu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya

2018 – Mchezaji Bora Kinda kwenye Kombe la Dunia, aliingia pia kwenye kikosi bora cha michuano hiyo

2018 – Mchezaji Bora wa Mwaka Ufaransa

2018 – Alipigiwa kura na mashabiki kuingia kwenye kwenye kikosi bora cha mwaka cha Uefa.com

2018/19 – Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

 

MENGINEYO;

Mbappe ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa tangu 2017. Hadi sasa amefunga mabao 13 katika michezo 33.

Mchezaji mdogo zaidi kufikisha mabao 10 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (miaka 18 na siku 350).

Mchezaji Kinda wa pili baada ya Pele kufunga bao kwenye fainali ya Kombe la Dunia

Ufaransa.

Monaco aliifungia mabao 27 katika mechi 60, wakati PSG hadi sasa ameshaifungia mabao 78 katika mechi 105.

Hadi sasa katika maisha yake yote ya soka, ameshafunga mabao 109 katika michezo 177.

PARIS, Ufaransa

Leave a Comment