×

JPM Asajili Laini ya Simu Kwa Vidole, Aongeza Siku 20 – Video

Rais John Pombe Magufuli akisajili laini yake ya simu kwa njia ya alama za idole mjini Chato mkoani Geita leo Desemba 27, 2019.

Rais John Magufuli leo Desemba 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole mjini Chato mkoani Geita na kuwasisitiza Watanzania wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

…Akielekea katika ofisi ya usajili wa simu.

Pamoja na kufanya hivyo, rais ameongeza siku 20 kuanzia Januari 1 hadi Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.

 

Leave a Comment