
Rais John Magufuli leo Desemba 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole mjini Chato mkoani Geita na kuwasisitiza Watanzania wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Pamoja na kufanya hivyo, rais ameongeza siku 20 kuanzia Januari 1 hadi Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.
