×

Anaswa na Dawa za Ukimwi Akisema Alitaka Kuwapa Ng’ombe

 

POLISI wilayani Igunga mkoani Tabora wanamshikilia mfamasia wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Francis Mlesa (33), kwa tuhuma za kuiba dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) na kwenda kuwauzia wafanyabiashara kwa ajili ya kunenepesha ng’ombe.

 

“Nilimuona anatoka na baiskeli akiwa amefunga mabox mawili saa 1:30 usiku nikamsimamisha na kumhoji akasema zimeisha muda wake wa matumizi, nilipokagua nikagundua hata mwaka wa kuisha haujafika, baada ya kumbana akakimbia, alisema Rushinangeme Paulo, Mlinzi.

 

Baada ya msako mkali, polisi wamemkamta mtuhumiwa ambaye anahojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.

Leave a Comment