×

Manara: Hatuwadharau Yanga, Buku 7 Kuiona Mechi Taifa – Video

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara,  akiongea na wanahabari.

MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kwamba timu hiyo haiwezi kuidharau timu ya Yanga ambayo watacheza nayo siku ya Jumamosi  hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Manara aliyesema hayo leo Januari 1, 2020 alipokuwa akiongea na wanahabari ambapo alifuatana na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa,  walipozungumzia kuhusu mchezo huo wa Simba dhidi ya Yanga.

 

Akizungumzia kiingilio katika mchezo huo, Manara amesema:-  “Tiketi katika majukwaa ya mzunguko  zitakuwa Sh. 7,000, VIP B&C – 20,000 na VIP A – 30,000. Sisi tutakuwa wenyeji wa mchezo. Nawaomba wana-Simba tununue tiketi mapema na tujitokeze kwa wingi. Lengo letu ni kwamba zaidi ya asilimia 70 ya uwanja tuwe sisi wana-Simba.

 

“Tumewafunga mara nyingi lakini hatuwezi kuwadharau japo sisi tumewazidi. Tunakwenda kupambana kutafuta alama tatu kama ilivyokuwa mechi ya jana ya Ndanda,” alisisitiza.

 

Chama cha soka nchini (TFF) kimemteua Jonesia Rukyaa kuwa mwamuzi wa kati, Sudi Lila atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Hamis Changwalu ambaye atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili na Eli Sasii mwamuzi wa akiba.

 

Kamishna wa mchezo atakuwa ni Khalid Bitebo, na mtathmini waamuzi ni Sudi Abdi.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa.

 

Naye  Mazingisa amesema: “Mwaka 2020 tunaanza na Yanga. Kama klabu tupo tayari, tupo tayari kwa maandalizi, tupo tayari kwa mchezo.

“Kabla hatujasajili tunahusisha wahusika wote. Tunalifanyia kazi sana hilo. Tunategemea kabla ya wiki kwisha tutatangaza mchezaji mpya.”

Leave a Comment