×

Askari Polisi Akatwa Nyeti na Mkewe kwa Madai ya Kuchepuka


JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanamke Frola Adamu (23), mkazi wa Shinyanga mjini, kwa tuhuma za kumkata mume wake sehemu za siri Askari Polisi mwenye namba H, 8980 Pc Kazimiri, kwa madai ya kumtuhumu ana nyumba ndogo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Deborah Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Decemba 28 mwaka jana, majira ya saa 6;30 usiku wakati Askali huyo akiwa wamelala na mke wake.

 

Alisema askari huyo akiwa amelala na mke wake, gafla mwanamke aliinuka na kuanza kumnyatia huku akiwa ameshika kitu chenye ncha kali, na kisha kumkata mume wake sehemu za siri na kumjeruhi vibaya.

 

“Baada ya askari huyu kukatwa uume wake alikimbizwa kwenye hospitali ya rufani ya mkoani Shinyanga ili kupatiwa matibabu ya haraka, ambapo alilazwa kwa muda wa siku mbili na kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea kujiuguza na kidonda,”alisema Magiligimba.

 

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, ambapo mwanamke alikuwa akimtuhumu mumewe kuwa ana nyumba ndogo, ndipo akaamua kuchukua kitu chenye ncha kali na kisha kuanza kuukata uume wa askari na kumjeruhi vibaya,”aliongeza.

 

Kamanda alisema Jeshi la Polisi bado linamshikilia mwanamke huyo, na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma ambazo zinamkabili.

 

Leave a Comment