×

Mmyika Amwangukia JPM: Msamehe Kabendera – Video

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amemuomba Rais John Magufuli amsamehe mwandishi wa habari wa kujitegemea, Erick Kabendera, ambaye anaendelea kusota rumande huku akikosa ruhusa ya mahakama ya kwenda kuzika mwili wa mama yake mzazi, Bi. Verdiana Mujwahuzi.

Mnyika ameyasema hayo leo Ijumaa, Januari 3, 2019, wakati alipohudhuria  ibada ya kuuaga mwili wa mama huyo mzazi wa Kabendera.

 

 

Mwili wa Verdiana umeagwa leo jijini Dar es salaam, katika Kanisa la Mtakatifu Francis Xavier Chang’ombe Temeke na utasafirishwa kuelekea Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya maziko.

 

Leave a Comment