
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, LOATA SANARE amekagua gwaride maalum la kuwapongeza na kuwapa zawadi askari sita waliofanya vizuri katika matukio mbalimbali likiwemo tukio la hivi karibuni la kumuokoa mtoto na baba yake (Benson Bernard Sadala Shila) waliokutwa kwenye maporomoko ya maji huku baba huyo akidaiwa kuwa alitaka kumjeruhi mtoto.