×

China Yagoma Kutoa Data za Covid-19 kwa WHO

 

CHINA imekataa kutoa data muhimu kwa timu ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inayochunguza asili ya Covid-19, ambapo mmoja wa wanachama wa shirika hilo alisema. kwamba huo ”ni utaratibu wa kawaida”.

 

 

Dkt Dominic Dwyer aliiambia Reuters, Wall St Journal na New York Times, kuwa timu hiyo iliomba data ya mgonjwa mpya kutoka kwa wagonjwa wa awali, kile alichokiita “mazoezi ya kawaida” lakini walipokea muhtasari tu.

 

 

Kwa upande wake, Serikali ya China haijajibu madai hayo lakini hapo awali imesisitiza ilikuwa wazi kwa WHO huku Marekani ikiitaka China kutoa data zinazopatikana kutoka katika hatua za mwanzo za mlipuko, ikisema ina “wasiwasi mkubwa” kuhusu ripoti ya WHO.

 

 

Wiki iliyopita, timu ya WHO ilihitimisha kwamba “haiwezekani kabisa” kwamba virusi vya corona vilivuja kutoka kwenye maabara katika jiji la Wuhan, ikiondoa nadharia yenye utata iliyoibuka mwaka jana.

 

 

Wuhan ilikuwa mahali pa kwanza ulimwenguni ambapo virusi hivyo viligunduliwa, mwishoni mwa 2019. Tangu wakati huo, zaidi ya watu milioni 106 wamepata maambukizi na vifo vya watu milioni 2.3 vimeripotiwa ulimwenguni.

 

 

WHO ilitaka kuona nini?

Wachunguzi walikuwa wanaomba data za watu 174 waliombukizwa Covid-19 kutoka Wuhan mwezi Desemba 2019, Profesa Dwyer aliiambia Reuters.

 

 

Prof Dwyer alisema vizuizi vya kupata data vitatajwa katika ripoti ya mwisho ya timu ya WHO, ambayo inaweza kutolewa mapema wiki ijayo. Timu hiyo ilikutana mapema Januari na ikakaa wiki nne nchini China – mbili za kwanza katika karantini hotelini.

 

 

China imesema nini?

Beijing imesisitiza kuwa ilikuwa wazi na wachunguzi wa WHO, ambao ziara yao ilianza tu baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa. Wataalam walikuwa wakifuatiliwa kwa karibu na mamlaka ya China.

 

 

Marekani iliilaumu China kwa kuficha kiwango cha mlipuko wa mwanzo na kukosoa masharti ya ziara hiyo, ambayo ilizuia uhuru wa timu ya WHO kusafiri na kuhoji mashahidi, pamoja na wanajamii, kwa misingi ya afya.

 

 

Leave a Comment