×

7 Wakamatwa Mwanza Wakidai Watumishi Ikulu

Watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi  baada ya kukamatwa jijini Mwanza.

POLISI mkoani Mwanza wanawashikilia watu saba kwa tuhuma ya kujifanya watumishi kutoka ofisi ya rais (Ikulu) kwa kinachodaiwa kufanya utapeli na kujipatia fedha  na kuwatishia baadhi ya wananchi katika mkoa huo ili wajipatie fedha, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Gari la kubebea wagonjwa linalodaiwa watuhumiwa walikuwa wanalitumia kufanya utapeli na kujipatia fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP. Muliro Jumanne,  amesema watu hao watafikishwa mahakamani huku akiwaomba wananchi na wakazi wa Mwanza kuendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa jeshi hilo ili liweze kuwakamata watu wanaofanya utapeli au vitendo vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

“Watuhumiwa walikuwa wakitumia gari la kubebea wagonjwa lenye namba za usajili T.751 BNL ambalo huwa wanaunga nalo nyuma ya misafara ya viongozi Wakuu wakijifanya ni sehemu ya Misafara, tumewakuta na vitambulisho vya Ikulu, pia na vinavyoonesha ni Marubani wa Ndege ya Rais,” amesema RPC Shanna.

Leave a Comment