×

Miguna Atolewa Kwenye Ndege ya Ufaransa kwa Amri ya Serikali

SHIRIKA la Ndege la Ufaransa (Air France) jana limemshusha kwenye ndege Mwanasheria Miguna Miguna aliyekuwa akielekea Nairobi likidai ni kwa amri ya Mamlaka za Kenya.

 

Hatua hiyo inayodaiwa ni kwa amri ya Mamlaka za Kenya inakinzana na taarifa ya awali iliyotolewa na Msemaji wa Serikali ya Kenya kuwa Miguna yupo huru kurejea Kenya.

 

Miguna alithibitisha kutolewa kwenye ndege AF0814 muda mchache kabla ya kuruka katika uwanja wa Charles De Gaulle huku akidai kuwa hajarudishiwa nauli yake.

 

Air France ilisema; “Kama ilivyo kwa mashirika yote ya ndege, tunatakiwa kufuata mahitaji ya kuingia kwa nchi tunazitumikia na kwa hivyo haturuhusiwi kupakia abiria wasioruhiwa kuingia nchi husika.”

 

Air France linakuwa Shirika la pili kumzuia Miguna kutumia ndege zake baada ya Shirika la Lufthansa kumzuia kutumia ndege zake jana katika uwanja wa TXL Airport huko Berlin, Ujerumani.

 

Leave a Comment