×

Washindi Tuzo za CAF Hawa Hapa, Diamond Apiga Shoo -Video

Samuel Eto’o .

USIKU wa kuamkia leo shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa tuzo mbalimbali za soka barani Afrika zilizofanyika Hurghurda nchini Misri.

 

Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz,  amenogesha sherehe hizo kwa kutumbuiza kwa mara ya pili katika tuzo hizo ambapo aliwapagawisha wageni waliofika katika ukumbi huo  ambapo mchezaji nyota wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o, aliyekuwa mshereheshaji,  na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora za soka barani Afrika,  Sadio Mane wa Cameroon,  wakishindwa kujizuia na kuungana na wengine kwa kucheza wimbo wa Yope.

Mane aliyetangazwa usiku wa kuamkia leo (Jumanne) kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2019, aliisaidia klabu yake ya Liverpool ua Uingereza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akiliongoza pia taifa lake la Senegal kufika fainali ya mataifa Afrika(‘Afcon).

 

Tuzo nyingine zilienda kwa Achraf Hakimi, ambaye anaichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mkopo akitokea Real Madrid, ambapo amekuwa mchezaji chipukizi bora wa soka wa mwaka 2019.

Aliyeibuka kuwa kocha bora wa mwaka ni Djamel Belmadi baada ya kuiongoza Algeria kubeba ubingwa wa Afcon mwaka 2019.

Kikosi bora cha soka Afrika kwa mwaka 2019 ni: Andre Onana; Serge Aurier, Joel Matip, Kalidou Koulibaly, Achraf Hakimi; Idrissa Gana Gueye, Riyad Mahrez, Hakim Ziyech; Mohamed Salah, Pierre Emerick Aubameyang, Sadio Mane

 

TUZO NYINGINE 2019

Mchezaji bora wa mwaka wa ndani: Youcef Belaïli (Algeria & Esperance / Ahli Jeddah)

Timu bora ya mwaka kwa wanawake : Cameroon

Timu bora kwa wanaume ya mwaka: Algeria

Goli bora la mwaka : Riyad Mahrez (Algeria)

Kocha bora wa kike wa mwaka: Desiree Ellis (South Africa)

Rais bora wa klabu Afrika: Moise Katumbi (TP Mazembe)

Mchezaji bora wa kike Afrika : Asisat Oshoala (Nigeria & Barcelona)

Leave a Comment