
FAMILIA ya kifalme ya Uingereza imesikitishwa na maamuzi ya mwanamfalme (Prince) Harry na mkewe Meghan kutangaza ‘kuacha’ kujihusisha na shughuli za kifalme ikisema haikuhusishwa na wala haikuwa na taarifa zozote za awali kuhusu maamuzi ya wanandoa hao.
Shirikala utangazaji la Uingereza (BBC) limsema limebainisha kuwa si Malkia wala Mwanamfalme William au waandamizi wengine katika ufalme huo walijulishwa hatua hiyo na kwa kwamba uongozi wa juu wa ufalme umepata pigo.
Habari zaidi zinasema suala hili ni gumu na wamelipokea kwa mshtuko mkubwa. Mwandishi wa zamani wa BBC kuhusumasuala ya kifalme, Peter Hunt, ameliambia BBC: “Mara nyingi huwa ninapata hofu kutumia neno ‘haijawahi kutokea’ ingawa sina mfano ambao ninaweza kufikiria kusema kuwa familia ya kifalme iliwahi kujisafisha katika jambo kama hili kwa umma.”

Katika maelezo yao, Harry na Meghan walisema kuwa walifikiria uamuzi huo kwa muda mrefu na kufanya maamuzi hayo miezi mingi iliyopita.
Harry na Meghan wamepanga kugawa muda wao kwa nusu kuishi Marekani na nusu Uingereza kuendelea kumtumikia malkia na kujihusisha na shughuli za kifalme.
“Maamuzi hayo yataturahisishia kumlea mtoto wetu katika makuzi ya utamaduni wa kifalme, na kuipa fursa familia kuangalia hatua inayofuata,” walisema wapenzi hao.

Msemaji wa zamani wa Malkia, Dickie Arbiter, alisema hafahamu ni namna gani wataweza kugeuza mipango yao. “Hii ni kama ndoto. Kuna suala la usalama: Nani atatoa ulinzi kwao?” alisema.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Mwanamfalme Harry na mkewe wametoa utetezi wao kuhusiana na tangazo lao kwamba hatua hiyo wameifikia baada ya kuwa na majadiliano ya ndani ya nyumba yao wao wawili kwa miezi kadhaa. Maamuzi yao yamepingwa kwa kudaiwa kuwa walistahili kupewa idhini ya jambo hilo na kutoa taarifa kabla.