
JAMAA mmoja aliyefahamika kwa jina la Boniface Mutuku Munyao wa Kangundo, Machakos nchini Kenya, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mbwa wa jike kisha kumuua usiku wa kuamkia Alhamisi, Januari 9, 2020.
Kwa mujibu wa taarifa, majirani usiku walisikia vilio vya uchungu visivyo vya kawaida toka kwa mbwa huyo ndipo wakapata na wasiwasi kuwa si bure kulikuwa na kitu kinaendelea.

Baadaye majirani walivunja mlango na kuingia wakamfuma mbwa huyo akiwa tayari kafariki dunia huku condom mbalimbali zikionekana kutumika.
Jamaa huyo anadaiwa ilikuwa tabia yake kumnyanyasa kingono mbwa huyo kwa kufanya naye mapenzi kwa siku tofauti ambapo inadaiwa zilikutwa kondomu kadhaa ndani kwake alizokuwa akitumia wakati akifanya tendo hilo la aibu.