
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kuanzia leo katika mikoa saba ambayo ni Singida, Rukwa, Mbeya, Njombe, Songwe, Dodoma na Iringa.
Taarifa ya Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuzingatia tahadhari ili kuepuka madhara mbalimbali yanayoweza kutokea.
Baadhi ya athari zinazoweza kutokea ni pamoja na makazi kuzungukwa na maji, changamoto ya usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.