×

Familia ya Kifalme Kumweka ‘Kati’ Prince Harry, Meghan

MALKIA wa Uingereza ameitisha mkutano na wanafamilia wa ngazi za juu wa kifalme leo Jumatatu, 13, 2020, katika eneo la Sandringham kwa lengo la kujadili muafaka wa baadaye wa watawala wa Sussex ana kwa ana.

 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kasri la Malkia kwenda kwa Shirika la Utangazaji la BBC, mkutano huo utahudhuriwa na Prince Harry  na kaka yake William mtawala wa Cambridge na baba yake Prince Charles, mtawala wa Wales huku mkewe Prince Harry, Meghan akitarajiwa kujiunga katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu kutokea Canada.

 

Watawala hao wa Sussex wiki iliyopita walitoa waraka uliosema wanajitoa katika nafasi ya kuwa wanafamilia wa juu wa kifalme sanjari na kuangalia namna ya kujitegemea kiuchumi huku wakiendelea kuheshimu taratibu za kifalme na malkia kwa ujumla.

 

Mpaka sasa hakuna hitimisho lililotolewa kuhusu mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kesho, lakini kwa mujibu wa mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya kifalme wa BBC, Jonny Dymond, amesema, ana matumaini kuwa mazungumzo hayo yatatoa picha ya baadaye ya mapendekezo ya wawili hao na uhusiano uliopo katika familia ya kifalme huku malkia akitamani kupata suluhisho ndani ya siku hizi chache na kuongeza kuwa bado kuna vikwazo vinavyoonekana huenda vikajitokeza katika mazungumzo hayo.

 

Wakati huohuo,  Mtawala wa Cambridge amezungumza na kueleza kusikitishwa kwake na kuvunjika muunganiko uliokuwepo kwao kama kaka, kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times.

 

Gazeti hilo limesema, Prince William amemueleza rafiki yake kuwa: “Nimekuwa nikimkumbatia mikononi mwangu kaka yangu wakati wote wa maisha yetu na sintaweza kufanya hivyo tena, tumeshatenganishwa na majukumu.

 

“Tunachoweza kufanya, na nitakachofanya, ni kujaribu kuwasaidia na ninatumaini wakati utafika wote tutaimba kutoka katika ukurasa mmoja.”

Leave a Comment