
IKIWA zimepita siku kadhaa baada ya Baraza Kuu la Madiwani Dar es Salaam kufanya mkutano na kumvua wadhifa wake, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo Jumatatu, Januari 13, 2020, amejikuta akishindwa kuingia ofisini kwake baada ya kukuta nywila (password) ya mlango wa kuingia ofisini kwake imebadilishwa na kulazimika kukaa nje.
“Nimekuja ofisini kwangu kuendelea na majukumu yangu ndiyo nimekuta hali hii,” amesema Mwita.
Mwita ambaye alivuliwa umeya kwa madai ya kutumia madaraka vibaya huku Mahakama ya Kisutu nayo ikitupilia mbali pingamizi lake, jana, Jumapili, alihudhuria ibada ya misa katika Kanisa la mchungaji Bendera lililoko Kimara Bonyokwa na kufanyiwa maombi mazito kufuatia figisu anadoai kufanyiwa na baadhi ya viongozi wenzake.
TAZAMA TUKIO ZIMA LA MAOMBI