

Marehemu Ajali Rashid Akbari alizaliwa January 25,1961 na kukutwa na umauti mnamo Januari 15 mwaka huu ambapo taarifa ya kifo chake iliyoelezwa na katibu wa bunge Steven Kagaigai imeeleza kuwa mbunge huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kifo chake.
Spika wa bunge Job Ndugai amemuelezea mbunge huyo kuwa alikuwa mbunge mwenye kupigania maslahi ya wananchi wake hasa kwenye sekta ya maji na nishati.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na wenye ulemavu Jenister Mhagama akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali amesema kuwa mbunge huyo wakati wa uhai wake aliungana na serikali katika jitihada za kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo la Newala vijijini.
Marehemu akbar ameacha mjane na watoto wanne na amezikwa nyumbani kwake Newala mkoani Mtwara.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.