The House of Social Media
gunners X

Butiku Aeleza Mtazamo wa Haki Kwenye Mgogoro wa CHADEMA

0

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu Januari 19, 2026, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation, Mzee Joseph Butiku, ameonesha kutofurahishwa kwake na misukosuko inayoikumba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mzee Butiku ameeleza wasiwasi wake kufuatia hatua ya chama hicho kuzuiwa kufanya shughuli zote za kisiasa na kiutendaji, hali inayosubiri uamuzi wa kesi ya madai inayoendelea mahakamani.

Katika maelezo yake, amesema iwapo chanzo cha tatizo kinahusishwa na mtu mmoja au viongozi wachache, akiwataja akina John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Tundu Lissu, Mwenyekiti Taifa, au kiongozi mwingine yeyote, basi ni vyema sheria ichukue mkondo wake kwa kumshughulikia mhusika husika.

Amesisitiza kuwa si haki adhabu kuigusa chama kizima chenye mamilioni ya wanachama kutokana na makosa au mgogoro unaodaiwa kuhusisha mtu mmoja au viongozi wachache, akiongeza kuwa hatua kama hiyo inaweza kuathiri misingi ya haki, demokrasia na ushiriki wa wananchi katika siasa.

Leave A Reply