×

Hakiki Laini Yako ya Simu Hapa Kama Imesajiliwa kwa Alama za Vidole

ZIKIWA zimebaki siku tatu laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kufungiwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaagiza Watanzania waliokamilisha usajili wa laini zao kuhakiki upya kwa kupiga namna *106#.

 

Taarifa kwa umma iliyotolewa juzi Alhamisi Januari 16, 2020,  na TCRA, imeeleza shughuli hiyo inapaswa kufanyika kabla ya kazi hiyo kuzima rasmi simu ambazo hazijasajiliwa Januari 20, 2020.

 

TCRA imesema ukomo wa Januari 20, 2020,  unawahusu wale tu ambao wana laini za simu sasa (ama kwa ajili ya mawasiliano ya simu au vifaa vyao vya mawasiliano mengine) lakini hawajazisajili kwa kutumia namba ya kitambulisho cha taifa (Nida) na kuthibitishwa kwa alama za vidole.


Leave a Comment