
Baada ya Mtangazaji wa Radio Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ kusema kwamba msanii Rajabu Abdul ‘Harmonize au Harmo’ na mkewe Sarah Michelotti ni miongoni mwa ‘kapo’ za mabilionea, meneja wa msanii huyo, Beauty Mmary ‘Mjerumani’ amesema amefurahishwa mno na kauli hiyo. Meneja huyo amezungumzia ubilionea ambao watu wengi wanamtabiria Harmo japo akasema yeye anamuona ni wa kawaida tu.
“Kuhusu Harmo kuwa bilionea, naona ni mawazo ya watu wanavyomuona ila Harmo yupo kawaida sana, lakini mimi ni furaha yangu kusikia watu wakimtabiria makubwa. “Nashukuru sana kuona watu wanazidi kumpaisha, waendelee kumfanya awe juu siku zote,” alisema meneja huyo.
Mjerumani alisema amefurahishwa na ubalozi wa Kampuni ya Sayona alioupata Harmonize na kusema, watu hao kumchagua Harmo kuwa balozi wao hawajakosea, bali wamepata mtu sahihi.
STORI: KHADIJA BAKARI