Klabu ya Polisi Tanzania imepata ajali leo asubuhi Julai 9, 2021 wakati ikitoka mazoezini kurejea kambini huko Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa shuhuda [hakutaka jina lake litajwe] ameeleza kuwa, gari liliacha barabara na kugonga mti maeneo ya jirani na Kiwanda cha Sukari TTC ambako ndio Polisi Tanzania FC hufanyia mazoezi yao na walikuwa warudi mjini [Moshi] ambako ndio kwenye makazi yao.
“Basi la Wachezaji wa Polisi Tanzania limepata ajali baada kuacha barabara na kugonga mti wakati likirudi kambini baada ya mazoezi. Kuna baadhi ya wachezaji wameumia vibaya lakini tayari wameshakimbizwa hospitali.”

