
Mbunifu maarufu wa mitindo hapa nchini Ally Rehmtullah, jana alikuja na gia mpya kwa kufanya hafla ya kuwaunganisha wabunifu wa vazi la kitenge na kufanya nao kazi pamoja.

Akizungumza na mwandishi wetu, Ally Rehmtullah amesema anawakaribisha wabunifu hao kufanyakazi zao kwenye duka lake lililopo Mtaa wa Chole, Masaki Dar na kuuzia kazi zao kwenye duka lake bila gharama yeyote.
Amesema lengo la kuwaunganisha wabunifu hao ni kuwajengea uwezo na kubadilishana ujuzi ili kuendeleza fani hiyo.





HABARI: Neema Adrian PICHA: Richard Bukos/GPL