×

Kortini kwa Kumbaka Mke Wake

MWANAMME mmoja, Nhlanhla Dlamini, mwenye umri wa miaka 34, amekuwa mtu wa kwanza kushtakiwa kwa madai ya ubakaji kwa kufanya tendo la ndoa na mkewe bila ya idhini yake nchini Eswatini (zamani Swaziland).

 

Kwa kutumia Sheria ya Makosa ya Kijinsia na Vurugu za Nyumbani (SODV) ya mwaka 2018, ambayo inakataza tendo la ndoa kati ya mume na mke bila ya kupatikana idhini, polisi walimtia mbaroni Dlamini na kumshitaki kwa kosa la ubakaji.

 

Siku ya Jumanne (14 Januari mwaka huu), Mahakama Kuu ya mji mkuu wa Mbabane ilimuachilia kwa dhamana ya dola za Marekani 3,400, na alitakiwa kurudi mahakamani wiki chache baadaye.

 

“Ni kesi ya kwanza kurekodiwa na kusikilizwa mbele ya mahakama ya wazi,” msemaji wa Kikundi cha Swaziland cha Hatua Dhidi ya Dhuluma (SWAGAA), Slindelo Nkosi, aliliambia shirika la habari la AFP.

WAUMINI MLIMA WA MOTO WALIVYOPEWA ZAWADI WOTE , “NI BARAKA ZA BWANA”

Leave a Comment