
MAPEMA leo Jumatano, Januari 22, mwaka huu timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya wafanyabiashara wa maeneo ya Mbezi, Kimara na maeneo mengine ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi zaidi.

Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo hayo wameonekana kuvutiwa na ujio wa gazeti hilo licha ya kuwasaidia katika masuala ya kubeti lakini pia jinsi linavyowapa fursa ya kutangaza nalo.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.
