
BUNGE la Burundi limepitisha sheria inatakayompa rais kitita cha Tsh. bilioni 1.15 atakapostaafu huku sheria hiyo ikiruhusu rais akistaafu atachukuliwa kwa hadhi ya makamu wa rais kwa kipindi cha miaka saba.
Bunge la Burundi limepiga kura kuruhusu Rais Piere Nkurunziza kulipwa US$ 500,000 (TZS Bilioni 1.15) anapojiandaa kuachia madaraka. Ametangaza kutogombea tena kiti hicho katika uchaguzi wa Mei mwaka huu. Nkurunziza atapatiwa pia mshahara maisha yake yote, nyumba na huduma kama za makamu wa rais.