×

Kijitonyama Veterans Yapata Mabosi Wapya

TIMU ya Kijitonyama Veterans wikiendi hii ilifanikiwa kupata viongozi wapya watakaoiongoza timu hiyo kwa kipindi cha miaka minne baada ya ya kufanya uchaguzi wake.

 

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Mwenyekiti aliyeshinda ni Lupiana Michael Lupiana ‘Rashford, Makamu Mwenyekiti ni Petro Malima ‘Sadio Mane.

 

Wakati katibu akiwa ni Amon Petro, Mratibu Majuto Omary, Mwekahazina Ally Feruzi ‘Teacher’ huku Ofisa Habari akiwa ni Wilbert Molandi.

 

Pamoja na viongozi wa kuchaguliwa, wajumbe wanne waliteuliwa kuunda Kamati ya Utendaji ambao ni Talib Chuji, John Mbitu ‘Morata’, Hamza Nzowa na Khalid Kahatano ‘Messi’.

 

Akizungumzia uchaguzi huo, Ofisa Habari wa timu hiyo, Wilbert Molandi alisema kuwa; “Baada ya uchaguzi huo, sasa hivi viongozi wote tunaelekeza nguvu zetu tunazielekeza katika kuifanya timu yetu inakuwa bora na yenye mafanikio na kikubwa kufikia malengo tuliyokubaliana katika kipindi hichi ambacho viongozi wapya wameingia madarakani.

Na Mwandishi Wetu

Leave a Comment