×

VANNESA: Niombeeni, nimebakisha ndoa tu!

MWANADADA Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka vigezo anavyovitaka kwa mwanaume anayetaka awe baba wa watoto wake ambapo amesema mwanaume aliyenaye sasa, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’ anavyo vigezo hivyo.

Vanessa amesema siku zote alikuwa anatamani aolewa na mwanaume ambaye ni mcha Mungu, mwenye mapenzi ya dhati kwake na pia atambue thamani ya mwanamke ambapo vyote mchumba wake wa sasa ametimiza hivyo vitu kilichobaki ni maombi tu ili ndoa iweze kufungwa.

“Siku zote nimekuwa nikitamani kuwa na mwanaume mwenye roho nzuri, sio yule ambaye akiwa na mimi anani- treat vizuri lakini akitoka huko nje anakuwa na roho mbaya, lakini pia awe na akili na mcha Mungu kwa sababu mwanaume akiwa na hofu ya Mungu anakuwa na heshima kwa wanawake, mpenzi wangu anavyo vigezo hivyo, tuzidi kuombeana,” alisema Vanessa.

Leave a Comment