Star wa muziki wa Singeli nchini Tanzania, Dulla Makabila ajitosa na kuachia muonekano wake mpya kike na kuwaacha wengi midomo wazi huku wengine wakimshambulia kwa matusi mazito.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Makabila ameposti picha hizo ambazo anaonekana amevaa wigi la kushoea, heleni, ametinda nyusi na kufanya make up, kisha kuandika kuwa “Ningekuwa Demu.”
Lakini baadae alikuwa kuposti tena teaser za wimbo wake mpya ambao ameuita ‘Ningekuwa Demu’.

