×

Mashabiki 30,000 wamvaa Mondi!

DAR: Zaidi ya mashabiki 30,000 wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, wamemvaa jamaa huyo wakimtaka aachie wimbo mpya.

Diamond au Mondi ndiye aliyewaomba mashabiki hao kutoa maoni yao haraka kwenye ukurasa wake wa Instagram juu ya kuachia wimbo mpya, ndipo walifanya hivyo kwa maneno makali.

Mondi alitupia kipande cha video kwenye ukurasa huo kikionesha ni cha video ya wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia, ambapo mashabiki hao walimtaka kufanya haraka ili kuwaziba midomo mahasimu wake kwenye Bongo Fleva.

“Queen Darleen mwambie kaka yako aachie wimbo wetu, komenti zimeshafika 30,000….(tusi)…Tunakuja makao makuu ya WCB (Wasafi Classic Baby),” ilisomeka moja ya komenti hizo.

Kwa upande wake, mama mzazi wa Mondi, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ alikwenda mbele zaidi na kumsisitizia Mondi kuachia wimbo huo haraka.

“Fumua Simba…” Aliandika Mama Dangote.

Komenti ya Mama Dangote ilikuwa ni kama kuchochea moto kwani mashabiki walicharuka na kumshambulia Mondi wakimtaka kumsikiliza mama yake.

“Mama Dangote ameshasema, sasa wewe Chibu (Mondi) unasubiria nini? Achia dude hilo,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo.

Stori: KHADIJA BAKAR, Ijumaa

Leave a Comment