×

Kili Canvas Yazinduliwa Rasmi Dar

Mwakilishi wa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Slivanus Mazula(kushoto) akimpongeza mshindi wa shindano la Sanaa ya uchoraji 2020, Athumani Hamis wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa picha aliyochora ikionekana nyuma yao iliyofanyika katika Hoteli ya Coral Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Shindano hilo lililiandaliwa na Kampuni ya Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020.

Dar es Salaam Februari 7, 2020: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager,  imezindua Kili Canvas itakayotumika kuhamasisha wakimbiaji wa vitongoji tofauti vya Jiji la Dar es Salaam na mji wa Moshi katika kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020 mkoani Kilimanjaro.

 

Hivi karibuni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia  Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager iliandaa shindano la uchoraji maarufu kama ‘“Jiachie na Kili Canvas Competition 2020’. Washiriki walitakiwa kuchora mchoro kwenye kitambaa kigumu (Canvas) kuelezea bia ya Kilimanjaro Premium Lager na mashindano ya riadha ya Kili Marathon.

Wasanii wa kikundi cha Bombeso wakicheza wakati wa hafla ya uzinduzi wa picha aliyochora na Athuman Hamis mshindi wa shindano la Sanaa ya uchoraji 2020 lililoandaliwa na Kampuni ya Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020.Hafla ya uzinnduzi ilifanyika katika Hoteli ya Coral Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Athumani Hamis kutoka Dar es Salaam aliibuka mshindi katika shindano hilo ambapo, mbali na kujishindia shilingi milioni mbili ambazo amekabidhiwa leo, alitakiwa kuchora  mchoro wa Kili (Kili Canvas) kwa ukubwa zaidi  kwaajili ya kutumika kama hamasa kuelekekea kilele cha Kili Marathon Machi Mosi mwaka huu, mkoani Kilimanjaro.

 

Washindi wengine ambao awali walikabidhiwa zawadi katika shindano hilo ni mshindi wa pili mpaka wa tano waliojinyakulia pesa taslimu shilingi 200,000/= kila mmoja, ambao ni Donath Kabonda (Gongo la Mboto), Moses Martin (Mwenge Vinyago), August Tairo (Kijitonyama) na George Nyandiche kutoka Morogoro Store Oysterbay.

 

Mshindi wa shindano la Sanaa ya Uchoraji, Athuman Hamis akizungumza kwa kushukuru na Wanahabari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa picha aliyochora, iliyofanyika katika Hoteli ya Coral Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi 2020.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa Kili Canvas itawekwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na baadaye mjini Moshi ili kuwahamasisha wakimbiaji mbalimbali kuelekea kilele cha Kili Marathon.

Alifafanua zaidi kuwa kutakuwa na Chip maalumu ambayo mkimbiaji atatakiwa kuwa nayo wakati akikimbia na atakapopita kwenye Canvas atapigwa picha na itatumwa moja kwa moja kwenye simu yake.

“Ili uweze kupigwa picha na kutumiwa kwenye simu yako kwa wale wakimbiaji ni lazima ujisajili na kupewa Chip maalumu ambayo utaelekezwa wapi pa kuiweka wakati unakimbia. Mara tu utakapopita karibu na Canvas kamera zetu zitakutambua na kukupiga picha kwa teknolojia maalumu na kutumiwa papo hapo kwenye simu yako” Kikuli alisema

Kwa mujibu wa Meneja huyo, usajili kwaajili ya kujipatia Chip hiyo ni kuanzia Februari 8 na 9, (Mlimani City), 13,14 na 15, (Shoppers Mikocheni na Mbezi) jijini Dar es Salaam.  Wakati Februari 15 na 16, 2020 itakuwa ni kwa wakaazi wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

“Kadi hizi zinapatikana kuanzia leo kwa hapa Dar es Salaam pale Mlimani City. Mtu yeyote anayependa mchezo wa kukimbia au anayefanya mazoezi ya kukimbia, anaweza kujipatia Chip hii kwa kipindi hiki ambacho tunafanya hamasa kwaajili ya kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon,” alisisitiza Kikuli.

Aidha Kikuli alivitaja vituo vitakavyowekwa Canvas hiyo kuwa ni Masaki, Goba na Temeke kwa  Dar es Salaam na baadae kuhamia Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Katika hatua nyingine, Kikuli aliwapongeza washiriki wote waliojitokeza kushiriki shindano la ‘Jiachie na Kili Canvas Competition 2020’ lililofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu,  akisifu ubora wa kazi zao. “Washiriki wote walifanya vizuri ila mwisho wa siku tukapata mshindi mmoja kutokana na taratibu za shindano lenyewe. Nimuombe mshindi wetu kwamba, kwa kile kidogo tulichomzawadia akitumie kama chachu ya kuendeleza sanaa yake pamoja na wasanii wengine waliomzunguka.

Kwa upande wake, mshindi (Athuman Hamis) alisema “Sisi wasanii wa uchoraji tuna kila sababu ya kuwashukuru TBL kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kutuonyesha njia kama hii. Sanaa ya uchoraji imesahaulika muda mrefu ikilinganishwa na aina nyingine za sanaa. Kwa hiki nilichokipata naahidi kuwa balozi mzuri wa Kilimanjaro kupitia sanaa yangu ya uchoraji.”

Nae Jaji Mkuu wa Mashindano ya “Jiachie na Kili Canvas Competition 2020”, Nathan Mpangala, aliwapongeza TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro kwa kuiangalia Sanaa ya Uchoraji na kuwaomba kuendeleza mpango huo kwa miaka ijayo ili kutoa fursa zaidi kwa wasanii hao.

MWISHO

Leave a Comment