
Vilio na majonzi vilitawala leo Februari 14, 2020 wakati mwili wa Waziri wa zamani wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Iddi Simba ukizikwa katika Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni, Dar.

Maziko hayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo marais wastaafu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt Ghalib Bilal na wengineo.

Baada ya dua ya kumuombea marehemu huyo, Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), Shehe Hamisi Mataka alimuelezea marehemu huyo alivyofanya nae kazi kwa miaka tisa kabla ya kupatwa na umauti huo. Shehe Mataka alieleza jinsi marehemu alivyokuwa na hofu ya Mungu kipindi cha uhai wake.


HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL