×

Wananchi Chumbuni Zanzibar Wanufaika na Gari La Kubeba Wagonjwa

Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi,  Salum Pondeza akiliangalia kwa ndani gari la kubeba wagonjwa katika jimbo lake ambalo amewakabidhi wananchi.
Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi,  Salum Pondeza akiwa amepozi mbele ya gari alilowakabidhi wananchi wa jimbo lake.
Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi,  Salum Pondeza akifunga mlango wa gari hilo.

 

Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi,  Salum Pondeza amesema wakati wanaingia madarakani miaka mnne liyopita katika jimbo hilo kulikuwa na changamoto kubwa ya huduma za afya za mama na mtoto, uhaba wa maji na ubovu wa barabara ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa eneo hilo kwa zaidi ya miaka 15.

 

Pondeza almaarufu AMJAD  akizungumza katika mkutano huo amejinasib kuwa kabla hajamaliza kipindi chake cha ubunge tayari amekwisha tekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia mia moja katika Nyanja zote alizo ahidi ikiwemo mojawapo magari ya kubebea wagonjwa aliyokabidhi.

 

Amesema leo anakabidhi gari la dharula la kubebea wagonjwa alilolinunua kwa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 45 ambalo ni la kisasa na lina vifaa vyote muhimu vinavyohitajika wakati mgonjwa anaposafirishwa.

 

“Wana Chumbuni nataka niwaambie kazi mlizonituma nimekamilisha kwa asilimia mia moja baada ya hapa labda niwakopeshe tu ilani zijazo, na hili gari ninalokabidhi leo limekamilika kila idara unaweza hata kufanyiwa operesheni hapa maana lina mitungi mpaka ya oxygen,”. alisema AMJAD

 

Adha ya gari la kubebea wagonjwa iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa jimbo la Chumbuni Zanzibar  huenda ikawa historia baada ya mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ussi Salum Pondea  kutoa gari la kisasa la kubebea wagonjwa lenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 45, kwa ajili ya zahanati ya Karakana iliyopo jimboni humo.

 

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Masumbani Unguja uliokuwa na lengo la kuelezea utekelezaji wa ilani ya mwaka 2015-2020 mwenyekiti CCM mkoa wa mjini Talib Ally Talib amewapongeza mbunge wa jimbo hilo,mwakilishi na madiwani kwa utekelezaji wa ilani kwa asilimia mia moja.

 

Amesema wakati chama hicho kinaomba ridhaa ya kuwaongoza wakazi wa jimbo hilo mwaka 2015-2020 waliahidi kuwaletea huduma za maji safii na salama, waliahidi kujenga shule za kisasa, waliahidi huduma bora za afya, waliahidi barabara bora uongozi bora mambo ambayo yote wameyatekeleza kwa asilimia mia moja.

 

“Ndugu zangu wana Chumbuni nataka niwaulize swali maji mnapata au hampati? umeme upo au haupo? na huduma za afya zimeboreshwa au haizijaboreshwa?alisema Talib.

 

Kwa upande wake mwakilishi wa jimbo hilo Miraji Khamis Mussa amesema akishirikiana na mbunge wa jimbo hilo na madiwani wametekeleza ilani kwa kuwapatia gari la jimbo ambalo wamekuwa wakilihudumia wao wenyewe kwa kuweka mafuta bila kuwadai wananchi.

Hapa mnapotuona tumetekeleza ilani zote tukishirikana na mhe mbunge wa jimbo. Baadhi ya wanachi wa jimbo la Chumbuni wamemshukuru mhe Pondeza kwa utelezaji wa ilani ya chama hicho ambapo awali walikuwa wakipata shida kubwa ya maji ambayo iliwalazimu kuifuata umbali mrefu.

Leave a Comment