×

Benjamin Fernandes: Alivyopata ujuzi nje na kurejea nyumbani – Video

AKIWA  amekabiliwa na mtaji mdogo lakini akiwa na nia na dhamira, Benjamin Fernandes, alikuwa mjasiriamali nchini Tanzania akishughulikia huduma za kifedha kidijitali zinazowawezesha watu kuzitumia akaunti zao katika program tumizi (app) na kuwawezesha kufanya manunuzi bila mtandao.

Katika mazungumzo haya  ya  TEDxEustonk, anaeleza safari yake kurejea nyumbani, kutoka taasisi mbalimbali na fursa nyingi alizopitia nchi za nje, na maarifa aliyoyapata. Benjamin Fernandes ni mwalimu wa Kitanzania na mjasiriamali akiwa pia mtangazaji wa zamani wa kituo cha televisheni cha taifa.

Ana shahada ya Uzamili ya Uongozi katika Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Stanford na Program ya Juu ya Elimuj ya Biashara (Exec Ed)  kutoka  Harvard University Kennedy School of Government, aliwahi pia kufanya kazi na taasisi ya  Bill & Melinda Gates Foundation katika  Taasisi ya Dijitali.

Akiwa mpenzi mkubwa wa program yenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa cha elektroniki (Android)  na uunganishaji wa huduma za kifedha na teknolojia barani Afrika,   Benjamin ni mwasisi na Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Fintech’NALA’, inayotoa huduma  za kifedha zinazopatikana nje ya mtandao.

Mazungumzo haya yalifanyika katika hafla ya TEDx kupitia mkutano wa TED lakini ukiwa umetayarishwa na jumuia huru ya eneo husika.

Pata habari zaidi kupitia: https://www.ted.com/tedx

Leave a Comment