×

Mwili wa Baba Mzazi wa Mtume Mwingira Kuzikwa Pwani Leo

Mwenyekiti wa ChademaTaifa , Freeman Mbowe, akitia saini kitabu cha maombolezo katika msiba wa Mzee Elias Josephat Mwingira (Baba mzazi wa Mtume na Nabii Josephat Mwingira) leo tarehe 22 Febr. 2020, Kibaha Pwani.

Mazishi ya Elias Mwingira ambaye ni baba mzazi wa Mtume Josephat Mwingira yanafanyika leo Jumamosi Februari 22, 2020 Kibaha mkoani Pwani.

Elias Mwingira alifariki dunia Januari 22, 2020 akiwa na umri wa miaka 94.

Katibu Mkuu wa Chadema, John Myika akitia saini kitabu cha maombolezo katika msiba wa Mzee Elias Josephat Mwingira (Baba mzazi wa Mtume na Nabii Josephat Mwingira) leo tarehe 22 Febr. 2020, Kibaha Pwani.

Ibada ya mazishi imeanza saa 4 asubuhi na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Leave a Comment