×

Amuua Mkewe kwa Mkuki Akiwa Amelala

HAWA JUMA (35) mkazi wa Kijiji cha Isikizya, Wilayani Uyui, ameuawa alipokuwa amelala kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodaiwa kuwa ni mkuki na mumewe, Omari Mkuyu.

 

Mauaji ya mwanamke huyo yametokea usiku wa kuamkia Februari 25, 2020, mwaka huu baada ya kuibuka mzozo baina ya wanandoa hao unaohusishwa na wivu wa mapenzi.

 

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, ACP Barnabas Mwakalukwa, amesema uchunguzi unaendelea kufanyika huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani muda wowote.

 

Matukio ya wapenzi/wanandoa kuuana au kujeruhiana huku chanzo kikiwa ni mapenzi yenyewe (hususan wivu) yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

 

Leave a Comment