


Shirikisho la filamu Tanzania limekabidhi rasimu mpya ya katiba kwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambayo itakwenda kumaliza changamoto mbalimbali zilikuwa zikiikabili Tasnia hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi rasimu hiyo Rais wa shirikisho la Filamu, Simon Mwakifamba alisema kuwa katiba hiyo itakwenda kumaliza changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye tasnia ya filamu Tanzania.
“Tasnia ya filamu ilikuwa na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikisababisha wasanii kushindwa kuteneza filamu nzuri na mambo mbalimbali kwenye tasnia, Tekinolojia pamoja na Serikali waandaji Wa Sera,kanuni na sheria ambayo inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri katika tasnia hiyo.
“Pia Tasnia yetu ilivamiwa na watu ambao walikuwa na lengo la kutuchafulia ila baada ya katiba hii tutamaliza hili tatizo na wasanii kupata manufaa kupitia kazi zao” alisema Mwakifamba.
Kwa sasa tumeboresha mifumo mbalimbali ambayo itakayompa manufaa makubwa msanii na kuzidi kunufaika na kuweza kuendesha maisha yake.
Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Fialamu, Dk. Kiagho Kilonzo alisema mchakato huo ulianza mwezi wa tano mwaka jana na ulilenga kumnufaisha msanii pamoja na Sanaa yake kwa ujumla.
“Baada ya kuingia Bodi ya filamu nilikuwa na ziara ya kukutana na wadau wa tasnia ili kusikiliza changamoto zao na tukaona kuna haja ya kubadilisha katiba yetu” alisema
Stori: Neema Adrian.