×

Hakuna mshukiwa, mgonjwa wa Virusi vya Corona Nchini — Video

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

SERIKALI kupitia Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  imesema hadi sasa hakuna mshukiwa wala mgonjwa yeyote wa virusi vya Corona nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,  leo Februari  29, 2020, akizungumza wanahabari kuhusiana na tishio la ugonjwa wa virusi vya  Corona, unaojulikana kitalamu kama COVID-19 na namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na tishio hilo. 

Alichokisema Ummy Malimu:

“Hatua mbali mbali ambazo tumezichukua na tunaendelea kuzichukua, ni kuendelea na uchunguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wote, wanaoingia nchini kwenye mipaka yetu, vikiwemo viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu.

“Jambo kubwa ambalo tumelifanya  ni kuongeza idadi ya wataalam wa afya katika maeneo ya mipakani, ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi 100 ili kuimarisha ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini kupitia maeneo ya mipakani.

“Tumeimarisha uwezo wetu wa kupima sampuli kupitia maabara yetu ya taifa ya afya ya jamii, ambapo ipo katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Masuala ya Tiba (NIMR) kwa watu wote wanaohisiwa kuwa na viashiria au dalili za ugonjwa huu, ambapo ndani ya saa nne hadi sitga tunaweza kutoa majibu ya vipimo.

“Wizara tayari imeshawaelekeza waganga wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini kubainisha vituo vya kutolea matibabu kwa washukiwa wa COVID-19, endapo watatokea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba vituo hivyo vinakuwa na vifaa vyote muhimu vya kutolea huduma.”

Leave a Comment