×

TAMKO la Global Kusuhu Habari ya Aslay na Sonia

Global Publishers na Global TV Online ni chombo cha habari kinachofuata miiko ya uandishi wa habari, tumefanya coverage ya habari ya Aslay na mzazi mwenzake aitwaye Sonia kwa kufuata taratibu zote.

 

Sonia amezungumza mwenyewe kwa mdomo wake akielezea ugomvi na madai ya kupigwa na mzazi mwenzake huyo pamoja na kunyimwa pesa ya matumizi ya mtoto wao mchanga, hata mama yake mdogo na Sonia naye pia ameeleza hayo na mambo mengine mengi na mazito kuhusu ugomvi huo.

 

Ili kuhakikisha stori inakuwa balanced, tulimtafuta Aslay lakini hakupokea kabisa simu yake, tukamtafuta Meneja wa Aslay aitwaye Chambuso kwa njia ya simu ili atolee ufafanuzi kuhusu suala hilo, lakini alikataa kutoa ushirikiano na kujibu kwa dharau kuwa ‘achana na mimi’.

 

Cha kushangaza Aslay ameilaumu Global kwa kutoa habari hiyo huku pia mzazi mwenzake huyo akifanya mahojiano mengine na media nyingine na kukana kupigwa wala kuwa na ugomvi na Aslay.

 

Hapa chini ni comment za Sonia kwenye Instagram account ya Aslay akisisitiza kuwa amepigwa na Aslay na si mara ya kwanza kupigwa na Aslay. Sasa, unaweza kuona binti huyu alivyo ‘kigeugeu’.

 

 

Sisi kama chombo huru cha habari, hatuna ugomvi na msanii yeyote wala hatutafanya hivyo, kazi yetu ni kuripoti kinachotokea kwa kufuata miiko na weledi wa tasnia ya habari, bila kujali ni stori ya staa ama mtu wa kawaida, tutaendelea kufanya hivyo kila siku.

 

 

Leave a Comment