×

Singida: Lema Aachiwa kwa Dhamana

MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Arusha Mjini GodblessLema ameachiwa leo Machi 5, 2020, na ameenda kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Polisi (RCO) Arusha kama alivyotakiwa kufanya baada ya kupigiwa simu na polisi ambao walienda kwake na kumkosa.

 

Baada ya hapo alisafirishwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Singida ambapo alihojiwa akituhumiwa kutoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kuchonganisha jeshi hilo na wananchi.

 

Aidha, Katibu wa Chadema  Wilaya ya Singida Mjini, alisema Lema alimwambia kuwa kosa analodaiwa kutenda ni kutaja orodha ya watu 14 waliouawa Manyoni kwa kuchinjwa na kuchomwa moto.

 

Leave a Comment