MSANII mkongwe wa muziki wa dansi kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo, Koffi Olomide anayetamba na kibao cha ‘Papaa Ngwasuma’ ametua jijini Dar es Salaam leo ili kuwafurahisha mashabiki wa muziki kwa burudani ya kihistoria itakayofanyika ukumbi wa Mlimani City kesho Jumamosi.
Akizungumza na vyombo vya habari hii leo katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar, Koffii amesema amefurahi sana kufika Tanzania maana ni nchi yenye watu wakarimu na upendo.
“Mimi nimefurahi sana kufika hapa Dar es Salaam maana nchi hii imejaa watu wakarimu wenye upendo wa dhati lengo langu kubwa kubwa ni kufanya shoo ambayo kila shabiki na mpenda muziki ataifurahia. Hivyo watu wote wa Afrika Mashariki wanakaribishwa na wafike kwenye shoo maana mzuka wangu ni zaidi ya kirusi cha Corona.
Koffi ametoa ushauri kwa wasanii wa muziki wa dansi hapa nchini kufanya kile ambacho wanatakiwa kufanya katika muziki wao na si kufanya kitu kwa kuiga au kwa sababu fulani amefanya hivyo, kwani inaweza kuua muziki kwa namna moja ama nyingine.
Koffii amembatana na wanamuziki wengine kutoka katika bendi yake ambao atajumuika nao katika kutumbuiza shoo hiyo..
Stori: Memorise Richard na Happyness Masunga


