×

Mshindi wa ‘Pata Simu Ya Bure’ Apatikana!

ILE ofa baab’kubwa inayotolewa na magazeti Pendwa ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Mchanganyiko, Ijumaa na Risasi Jumamosi ya kujinyakulia simu ya kisasa (smart phone) imeanza kuzaa matunda baada ya mshindi wa kwanza kupatikana.

Mshindi huyo si mwingine ni Upendo Mbendela, mkazi wa Namanga, jijini Dar ambaye amekabidhiwa simu yake baada ya kushiriki ofa hiyo kwa kujibu kwa ufasaha maswali yaliyoulizwa katika ofa hiyo.

Akizungumza mara baada ya kufika kwenye ofisi za Global Publishers, Sinza-Mori jijini Dar wiki iliyopita, Upendo alisema amekuwa akisoma magazeti Pendwa tangu mwaka 2008 kutokana na kusheheni vitu vingi vya kuelimisha na kuburudisha.

“Nasoma yote kuanzia Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Mchanganyiko, Ijumaa na Risasi Jumamosi humo kuna machombezo, hadithi na saikolojia,” alisema Upendo na kuongeza:

“Nawasihi na watu wengine wote wazidi kusoma magazeti ya Global kwani mbali na kuelimika na kuburudika, utapata zawadi kama hivi simu na nyingine nyingi watakazokuwa wanatoa.”

Kwa maelezo ya jinsi ya kujinyakulia simu hizo, tazama kuponi ambayo ipo ukurasa wa pili au wa tatu katika magazeti Pendwa.

Leave a Comment