BURKINA FASO inakuwa nchi ya 10 Afrika kuthibitisha kuwa na wagonjwa wenye virusi vya Corona ambapo wagonjwa wawili wa kwanza wa Corona wamebainika nchini humo.
Wagonjwa hao ni wapenzi, mmoja ndiyo kwanza amerudi akitokea Ufaransa na ndiye aliemwambukiza mpenzi wake.
Burkina Faso inafanya idadi ya Nnhi za Afrika zilizokumbwa na Corona kufikia 10, nyingine ni Cameroon, Misri, Togo, Morocco, Senegal, Algeria, Nigeria, Afrika Kusini na Tunisia.

