×

Updates: Mbowe, Wenzake Wakutwa na Hatia Makosa 12

UPDATES KUTOKA KISUTU, HUKUMU YA MBOWE VIONGOZI WENZAKE:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani washtakiwa wote katika mashtaka 12, isipokuwa shtaka la kwanza ambalo ni kula njama katika kesi ya kina Mbowe.

 

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amesema shitaka la 5,6,7,8,9,10,11,12 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa ambao ni Freeman Mbowe na wenzake upande wa mashtaka umethibitisha pasipo shaka kwamba washtakiwa wana hatia.

 

“Maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi ambayo yalitolewa na watuhumiwa wote; Je, miongozo ya uchaguzi inaruhusu maneno hayo? Hapa hatuhitaji kuwauliza washtakiwa juu ya maneno hayo isipokuwa mahakama yenyewe ndiyo inapaswa kutafsiri maneno hayo kama yalivyo,” amesema Hakimu Simba.” Hakimu Simba, Kisutu.

 

“Mkutano wa Chadema ulikuwa halali kwa sababu walikuwa na kibali. Lakini watuhumiwa walipoanza kuondoka kutoka mahali ulipokuwa unafanyika kwenda Manispaa ya Kinondoni ndiyo walifanya mkusanyiko usio halali na kutotii sheria.” Hakimu Simba, Kisutu.

 

“Baada ya kufunga mkutano wa uchaguzi saa kumi na mbili, mkusanyiko kuelekea kwa Mkurugenzi wa Kinondoni haukuwa halali.”  Jaji Thomas Simba.

 

 

Wakili Kibatala amemwomba Hakimu kutoa hukumu ya washtakiwa walipe faini badala ya kuwapa adhabu ya kifungo baada ya washtakiwa wote kukutwa na hatia kwenye makosa 12 kati ya makosa 13 yaliyokuwa yakiwakabili.

Leave a Comment