The House of Favourite Newspapers

Wema, Mondi Gumzo Jipya Mjini

0

STAA wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na mwanamuziki mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ndiyo gumzo jipya mjini. Gumzo hilo limekuja siku kadhaa baada ya Diamond au Mondi kudaiwa kuachana na mzazi mwenzake Tanasha Donna Oketch.

 

Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyozungumza na gazeti la Risasi Mchanganyiko, vilidai kuwa, familia ya jamaa huyo inampigia pande Wema ili arudi mjengoni (arudiane na Mondi). Chanzo kimojawapo kimeliambia gazeti hili kuwa inaonekana familia nzima ya Mondi imerudisha ukaribu.

 

Mbali na ukaribu, dada wa Mondi, Esma Khan amekuwa akimmwagia Wema sifa kemkem kuwa ni mmoja wa wanawake wenye akili na kujielewa.

“Kama hujui ni kwamba familia nzima sasa inamtaka Wema na ndiyo maana inamtaja mara kwa mara hata wakifanya mahojiano na vyombo mbalimbali, yaani ninyi mtakuja tu kusikia Wema na Mondi wamerudiana,” kilisema chanzo kingine.

 

Kufuatia Mondi kumtaja Wema kuwa miongoni mwa ‘super woman’ Siku ya Wanawake Duniani, Jumapili iliyopita, mashabiki wao waliendelea kuunganisha nukta.

Katika kumjibu Mondi, Wema aliibua gumzo jipya baada ya kufunguka kupitia ukurasa wake wa Twitter; “You always have a special place in my heart and you know it.”

 

Baada ya kupata ubuyu huo, Gazeti la RISASI MCHANGANYIKO lilimtafuta Esma ambapo alipoulizwa juu ya familia yao kutaka kumrejesha Wema kwenye himaya ya Mondi, alisema kuwa, hawajawahi kugombana na Wema na kama ana jambo zuri, lazima wamsifie.

 

“Wema sijawahi kugombana naye hata kidogo, hana shida na mimi kabisa. Kwa nini nisimtaje kama ana jambo lake zuri jamani,” alisema Esma.

Kwa upande wake Wema alipoulizwa na gazeti hili juu ya ishu hiyo ya kurejesha majeshi kwa Mondi, alicheka mno na kusema hakuna kitu kama hicho, lakini pia hana ugomvi na familia hiyo.

 

“Leo umenifanya nicheke, kama wamenisifia ni sawa maana sina tatizo nao kabisa, lakini kwa kunipigia pande siyo kweli kabisa,” alisema Wema na kuachia kile kicheko.

 

Wema na Mondi waliwahi kuwa wapenzi, wakaachana, wakarudiana kisha wakaachana tena huku kila mmoja akieleza hisia za kumkubali mwenzake. Matendo yao yanaelezwa kuwa yanaelezea kile kilichomo mioyoni mwao na kwamba waliachana kimwili tu.

 

STORI: Imelda Mtema, Risasi

Leave A Reply