×

Binti wa Kazi Aliyeuawa Kisa Elfu 50, Aagwa! – Video

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho  Gambo, jana Alhamisi, Machi 12, 2020, aliongoza mamia ya waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Salome Zakaria Hoya katika viwanja vya Hosptali ya Mkoa ya Mount Meru mkoani humo ulipokuwa umehifadhiwa.

 

Salome (18) alifariki Jumanne, Machi 10, 2020 kwa madai ya kushushiwa kipigo kikali kutoka kwa  bosi wake, kufungiwa ndani na kunyimwa chakula kwa siku tatu akimtuhumu kuwa amemuibia pesa zake kiasi cha Tsh 50,000, lakini baadaye ikadaiwa kuwa pesa hizo alikuwa amezichukua mtoto wa bosi huyo wala siyo Salome.

 

Mwili wa marehemu Salome umesafirishwa kwenda kijijini kwao wilaya ya Manyoni mkoani Singida kwa ajili ya maziko.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

Leave a Comment