×

Z Anto Afungukia Ugomvi wa Wastara, Binti Kiziwi

IMEIBUKA stori hivi karibuni ambayo inaendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ugomvi wa video vixen Binti Kiziwi na msanii wa filamu Wastara Sajuki juu ya kumgombania Z Anto.

 

Taarifa hizo zimekuja baada ya Wastara Juma kumtishia kumchana na viwembe Binti Kiziwi endapo ataendelea kuwasiliana  na Z Anto mida ya usiku kwa sababu anamjua vizuri kuliko anavyomjua yeye.

 

Z Anto amefunguka na kusema: “Sitaki kuongea sana kuhusiana na hii ishu ila Wastara ni mtu mzima na ikifikia hatua ya kuongea kitu ambacho kipo serious sijui kuna nini, siwezi kuwa sawa kutokana na kinachoendelea mitandaoni na pengine watakuwa na hasira zao binafsi.”

 

Z Anto aliwahi kuwa kwenye ndoa na Binti Kiziwi, kisha kuachana baada ya miaka mitatu.

Leave a Comment